Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kurejelea usambazaji wa chakula kwa watoto wanaotaabika nchini Swaziland

WFP kurejelea usambazaji wa chakula kwa watoto wanaotaabika nchini Swaziland

Shirika chakula la Umoja wa Mataifa WFP litarejelea shughuli za usambazaji wa chakula kwa vituo 1600 vya huduma nchini Swaziland baada ya shughuli hiyo kuvurugwa mapema mwaka huu kutokana na ukosefu wa ufadhili.

Kulingana na WFP usambazaji huo wa chakula utawanufaisha mayatima 97,000 na watoto wengine 33,000 wanaotaabika. Asilimia kubwa ya watakaopokea chakula hicho ni mayatima ambao wazazi wao wameaga duniani kutokana na ugonjwa wa ukimwi.