Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa Haiti waishio kambini bado wakumbwa na madhila makubwa: IOM

Wakazi wa Haiti waishio kambini bado wakumbwa na madhila makubwa: IOM

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la uhamiaji duniani, IOM pamoja na mashirika yake imeonyesha madhila ambayo bado yanawakumba wakazi wa Haiti kufuatia majanga ya mfululizo yaliyokumba nchi hiyo kuanzia mwaka 2010.

Mathalani ripoti hiyo inaonyesha ukosefu wa ajira, watu kuendelea kuishi kwenye makazi na idadi kubwa ya kaya kuongozwa na wanawake pekee. Tupate taarifa zaidi na Alice Kariuki:

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)