Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya zisibugudhiwe wakati wa migogoro: WHO

Huduma za afya zisibugudhiwe wakati wa migogoro: WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema shambulio lolote dhidi ya wahudumu wa afya halikubaliki na kwamba migogoro au mapigano yoyote hayapaswi kubughudhi huduma za afya.

WHO imetoa kauli hiyo kufuatia kupigwa risasi na kuuawa kwa wafanyakazi sita waliokuwa wanaendesha kampeni ya polisi nchini Pakistan.

Shirika hilo limesema vitendo hivyo vikifanyika, wanaopata madhara ni watoto na jamii husika kwa kuwa chanjo hazitatolewa. Hata hivyo limepongeza utayari ulioonyeshwa na viongozi wa kijamii na wa serikali nchini Pakistani ambako mafanikio makubwa yamepatikana katika vita dhidi ya polio. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

(SAUTI YA TARIK)