Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi Mali vunjeni uhusiano na vikundi vya kigaidi: Azimio Baraza la Usalama la UM

Waasi Mali vunjeni uhusiano na vikundi vya kigaidi: Azimio Baraza la Usalama la UM

Kwa kutambua athari za mzozo wa mali kwa amani na usalama duniani, hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio ambalo pamoja na mambo mengine linataka waasi nchini humo kuvunja mara moja uhusiano na vikundi vya kigaidi ikiwemo Al-Qaida na kuthibitisha hatua hiyo.

Azimio hilo pia linataka mamlaka za mpito nchini Mali kukamilisha mpango shirikishi wa kuelekeza nchi hiyo katika mazingira tulivu ya kisiasa ikiwemo uchaguzi huru na wa haki wa rais na wabunge.

Halikadhalika mamlaka hizo zimetakiwa kuharakisha mchakato wa kuaminika wa mashauriano na vikundi vyote kaskazini mwa Mali ambavyo tayari vimekata uhusiano na magaidi.

Baraza pia limelaani matukio yote yaliyosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Mali na kuondolewa madarakani kwa serikali wiki moja iliyopita na kutaka vikosi vya kijeshi nchini humo visiingilie serikali ya mpito.

Mohammed Loulichki  ni Rais wa sasa wa Baraza la Usalama.

 

(SAUTI YA MOHAMMED)