Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wapalestina 100,000 waikimbia Syria

Zaidi ya wapalestina 100,000 waikimbia Syria

Maelfu ya wapalestina kwa sasa wanaendelea kuihama Syria kufuatia kuwepo mapigano makali yaliyotokea kwenye kambi ya Yarmouk mjini Damascus. Kambi hiyo ilishambuliwa kwa mabomu na ndege za kivita za Syria siku ya Jumapili kufuata tuhuma za kuwepo kwa waasi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestinba UNRWA linakadiria kuwa theluthi mbili kati ya wapalestina 150,000 waliokuwa kambi ya Yarmouk wamekimbia na kutafuata makao kwenye miji iliyo karibu pia sehemu za vijijini huku wengine wakielekea nchini Lebanon.

Lisa Gilliam ni afisa kutoka UNRWA