Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM lalaani mashambulizi huko Jamhuri ya Afrika ya kati

Baraza la Usalama la UM lalaani mashambulizi huko Jamhuri ya Afrika ya kati

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yaliyoendeshwa na  makundi yaliyojihami siku chache zilizopita kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya kati pamoja na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaondelea.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari wajumbe wa Baraza hilo pia wameelezea wasiwasi wao kutokana na hali ilivyo nchini humo wakisema kuwa usalama wa raia uko mashakani, halikadhalika uthabiti wa taifa hilo.

Wamesema wale wanaohujumu jitihada na kupatikana kwa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati watawajibika.

Pia Baraza la Usalama limeyataka makundi yaliyojihami kukomesha dhuluma, wajiondoe kwenye miji  na pia waache kusonga mbele kuelekea mji mkuu, Bangui.