Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaomba Kenya iendelee kulinda haki za wakimbizi

UNHCR yaomba Kenya iendelee kulinda haki za wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na matukio ya hivi karibuni nchini Kenya ya kuuawa kwa raia pamoja na wakimbizi.

UNHCR imesema inalaani mashambulizi hayo na kutoa rambirambi kwa waathirika wote, watu na serikali ya Kenya huku ikiomba serikali hiyo kuendelea kulinda haki za wakimbizi.