Usalama kambi ya Mugunga huko Goma si nzuri: Wanawake wapaza sauti zao

19 Disemba 2012

Umoja mataifa kupitia msimamizi Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous umetangaza bayana kuwepo kwa sintofahamu ya hali ya usalama huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Hali hiyo imeibuka baada ya kuondoka kwa waasi wa M23 mwanzoni mwa mwezi huu, lakini kumeripotiwa kuonekana kwa baadhi ya waasi hao pamoja na watu wengine wenye silaha katika maeneo ya mji wa Goma, hali inayoibua wasiwasi hata miongoni mwa wakazi wa kambi ya Mugunga iliyopo mji wa Goma. Ungana na Alice Kariuki kwa ripoti kamili:

Maisha katika kambi ya Mugunga ni magumu. Chakula hakitoshi, kwani raia wa DRC waliopoteza makazi yao na kukimbilia kwenye kambi hii wanahaha kutafuta chakula kwa familia zao. Kambi ya Mugunga iko takribani kilometa 15 Magharibi mwa Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, lililopo Mashariki mwa DRC. Mara kadhaa katika miezi iliyopita vikundi vya watu wenye silaha vilishambulia kambi hii na wanawake wengi waliripotiwa kubakwa. Licha ya hali hiyo, wakimbizi wengi wakiwemo wanawake wanawasili hapa kila siku wakikimbia mapigano kwenye vitongoji vyao.

(SAUTI YA MAMA KUTOKA MUGUNGA)

Kambi hii ina takribani wakimbizi Elfu Thelathini na wana matatizo lukuki:

(SAUTI YA MGONJWA-MUGUNGA)

Mashirika mbali mbali ya misaada ya Umoja wa Mataifa yakishirikiana na taasisi zingine yanajitahidi kutoa misaada mbali mbali lakini yanakumbana na changamoto za kupambana na vitendo vya ubakaji kama asemavyo Sabine Mubi wa taasisi ya kiraia ya ktoa misaada:

(MFANYAKAZI WA SHIRIKA LAKUTOA MSAADA)

"Wanawake hawana ufahamu wa kutosha hasa wakifika hapa. Kuna baadhi wana hofu ya kuficha kuwa walibakwa na hivyo wanaficha na hawafahamu kuwa ukibakwa hupaswi kujificha bali tafuta tiba. Kwa hiyo tunahitaji kuwaelimisha lakini pia tunahitaji usalama kwani wanawake wanabakwa kila siku.”

Lakini hali ya usalama iko vipi? Bishweka Edson ni Mkuu wa polisi kwenye kambi ya Mugunga.

(SAUTI)

Wanawake wanasema wamechoka kuishi kambini wanataka kurejea makwao wakaishi na watoto wao hivyo wanatoa ombi maalum.

(SAUTI YA MLINZI)

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani baada ya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani katiak umoja huo Herve Ladsous amekiri kuwepo kwa sintofahamu ya usalama huko Goma na kusema kuwa MONUSCO wanajiandaa kwa lolote iwapo M23 watarejea.

Naam ilikuwa ni ripoti ya Alice Kariuki kuhusu hali ya usalama katika kambi ya Mugunga huko Goma, mashariki mwa DRC.

(PKG)