Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ampongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea

Ban ampongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemtumia salamu za pongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea na kuelezea utayari wa kushirikiana na serikali mpya ya nchi hiyo.

Bi. Park, mtoto wa dikteta wa zamani nchini Jamhuri ya Korea Park Chung-hee,  ameibuka mshidni katika uchaguzi wa Jumatano na anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Urais nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akieleza kuwa Jamhuri ya Korea ni mshirika wa dhati na wa thamani kwa Umoja wa Mataifa katika utekelezaji wa majukumu ya ulinzi wa amani ya kimataifa, maendeleo na haki za binadamu.

Halikadhalika amesema yuko tayari kushirikiana na serikali hiyo mpya kuendeleza amani na utulivu katika rasi ya Korea kwa kushughulikia masuala kama vile nyuklia na yale yanayohusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea.