Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watafuta fedha zaidi kukabiliana na waasi wa LRA

19 Disemba 2012

Katika harakati za kukabiliana na vitendo viovu vinavyofanywa na kikundi cha waasi cha Lord’s Resistance Army kwenye maeneo ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinatafuta fedha zaidi kutekeleza mipango yake ya kudhibiti kikundi hicho.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Ya kati, UNOCA Abou Moussa amelieleza Baraza la Usalama kuwa jambo la haraka zaidi ni kukamilisha nyaraka ya mpango wa utekelezaji na hatimaye kuchangisha fedha za kutosha kutekeleza mpango huo. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter