Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO imejiandaa kwa lolote: Hervé Ladsous

MONUSCO imejiandaa kwa lolote: Hervé Ladsous

Tangu kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka mji wa Goma mapema mwezi huu, hali ya sintofahamu kuhusu usalama kwenye eneo hilo imeendelea kudumu katika mji huo mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini.

Kutokana na hali hiyo Msimamizi Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwa Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema MONUSCO ambacho ni kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko DRC kinabaki tayari kukabiliana na uwezekano wowote wa kurudi kwa waasi wa M23, ambao yasemekana wanazungukazunguka katika viunga vya mji wa Goma.

Amewaeleza waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Usalama kuwa kuzunguka hovyo kwa baadhi ya waasi hao na wengine kunatia wasi wasi na kusababisha ongezeko la walinda amani wa MONUSCO hasa katika kambi za wahamiaji wa ndani kwa lengo la kulinda raia.

(SAUTI YA HERVE LADSOUS)

Habari zinasema ubakaji wa hivi karibuni wa wanawake uliotekeleza na M23 unaathiri akili za watu wote. MONUSCO kwa upande wake, inafanya uchunuguzi na imeahili matokeo ya uchunguzi huo mapema mwezi Januari.

Mmoja wa wanawake katika kambi ya Mugunga namba Tatu Mashariki mwa DRC ameelezea hali inayowakumba.

(SAUTI YA MAMA KUTOKA MUGUNGA)