Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE yaidhinisha mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani

UNECE yaidhinisha mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani

Mkataba wa kimataifa wa matumizi ya vito vizito umepiga hatua baada ya kuungwa mkono na mataifa kadhaa kufuatia jitihada za majadiliano za miaka 3.

Mkataba huo ambao ni umeratibiwa na kamishna ya kitaifa inayohusika na masuala ya uchumi barani Ulaya UNECE umelenga kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani.

Kwa mara ya kwanza mkataba huo uliasisiwa mwaka 1998, na baadaye uliongezewa vipengee vingine vilivyolenga kuupa uhai zaidi.

Viongozi wa ngazi za juu kwenye kamishna hiyo baada ya majadiliano ya saa kadhaa hatimaye waliridhia kupitishwa kwa itifaki hiyo.