Ukosefu wa usalama mjini Goma wahatarisha maisha ya wakimbizi wa ndani

Ukosefu wa usalama mjini Goma wahatarisha maisha ya wakimbizi wa ndani

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya usalama kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mugunga 3 karibu na mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemeokrasi ya Congo ni ya kutia wasi wasi.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa wanajeshi na watu wasiotambulika wanaonekana nje na ndani mwa kambi suala ambalo huzua wasi wasi miongoni mwa wenyeji wa kambi.

Bwana Adrian amerejelea wito kwa UNHCR wa kutaka makundi yaliyojihama kuondoka kwenye maeneo hayo akisema kuwa raia ni lazima walindwe na pia hatua ya kupelekwa wanajeshi kwenye sehemu zenye watu wengi ni lazima ikomeshwe.