Mamia ya wanawake na wasichana wadhulumiwa kimapenzi Goma

18 Disemba 2012

Karibu wanawake na wasichana 400 walibwakwa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati wa mapigano ya hivi majuzi kweneye mji wa Goma. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa huduma inatolewa kwa wanawake 278 na wasichana 117 waathiriwa wa dhuluma za kimapenzi.

UNICEF inasema kuwa wanawake na wasichana kwenye kambi wanaishi na hofu ya kuvamiwa na kudhulumiwa. Pia Shirika hilo linasema kuwa linafanya jitihada za kuwaunganisha watoto 751 waliotenganishwa na familia zao wakati wa mapigano. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF mjini Geneva.

Washirika wetu wa kulinda watoto wameunganisha watoto 84 na familia zao kupitia mtandao wa kijamii. Watoto hawa wako kwenye hatari, hawana pesa hivyo wanaenda nje kwenye maeneo ya karibu wakati mwingine usiku kutafuta kuni wauze na hili huwaweka wasichana hawa kwenye hataii ya kubakwa na watoto wa kiume kwenye hatari ya kuingizwa jeshini. Hatari ya mkurupuko wa magonjwa pia inaongezeka. Kivu Kaskazini kumekuwa na zaidi ya visa 650 vya ugonjwa wa surua ikiwa ni mara kumi zaidi ya idadi ya mwezi Disemba mwaka uliopita. Hata baada ya kuwepo hali mbaya ya usalama watoto 27,000 waliohama makwao wamechanjwa kwenye kampeni ya pamoja na wizara ya afya, Merlin, , Médecins Sans Frontières amblo wamesema Visa vya ugonjwa wa kipindundu vinazidi kupanda pia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud