Vita dhidi ya Malaria yakwamishwa na pesa: Tanzania Zanzibar, Rwanda na Zambia zang’ara katika kutokomeza Malaria

17 Disemba 2012

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2012 imeonyesha kupungua kwa ufadhili katika mipango ya vita dhidi ya ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu takribani Laki Sita na Elfu Sitini duniani kote.

Idadi kubwa ya vifo hivyo ni vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha mafanikio katika baadhi ya nchi mathalani Tanzania upande wa Zanzibar ambapo maambukizi kwa sasa ni asilimia Sifuri.

Nchi zingine zilizofanikiwa ni Rwanda na Zambia ambapo mafanikio hayo yanatokana na hatua za kinga kama vile kutumia vyandarua vyenye viuatilifu pamoja na kupuliza dawa kuua mazalia ya mbu. Taswira mbili hizi za mafanikio na kupungua kwa ufadhili inaweka tishio la uwezekano wa kurejea kwa kasi kubwa ya Malaria iwapo ufadhili utapungua. Alice Kariuki na ripoti zaidi:

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud