Shambulio lingine nchini Iraq laua raia: Mjumbe wa Ban ataka pande husika zifanya mashaurino

17 Disemba 2012

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler, ameshutumu vikali msururu wa mashambulio ya jana na leo yaliyotokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 44 na wengine 77 wamejeruhiwa.

Habari zinasema katika shambulio la leo alfajiri kaskazini mwa nchi hiyo lililolenga askari wa jeshi la Iraq na raia, watu 25 wamekufa ambapo jana katika shambulio la jana kwenye jimbo la Kirkuk, watu 19 waliuawa na wengine 77 walijeruhiwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa na Ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI ambayo yeye ndiye kiongozi wake, Bwana Kobler ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu kwenye mashambulio hayo huku akiwatakia uponaji wa haraka wale waliojeruhiwa.

Amezitaka pande zote zinazozozana nchini Iraq zifanye mashauriano haraka kuondoa mvutano. Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kufanikisha mazungumzo hayo iwapo utaombwa kufanya hivyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter