UNHCR kuanzisha kituo Jordan kuwafadhilia wakimbizi wa Syria

17 Disemba 2012

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi António Guterres ametangaza kuanzishwa kwa kituo cha pamoja kitaratibu misaada ya kibinadamua kwa mamia ya wananchi wanaokimbia mapigano nchini Syria ambao hadi sasa wamefikia 250,000 waliopata hifadhi nchini Jordan.

Kituo hicho ambacho kitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Jordan kinalenga kukabiliana na tishio la kuzuka kwa baa la kibinadamu kutokana na kushadidi kwa machafuko nchini Syria mapigano ambayo yamezusha hali ya wasiwasi kwa mataifa jirani.

Duru za habari zinasema kuwa kunauwezekano eneo hilo likashuhudia mkwamo zaidi katika kipindi cha katikati mwakani iwapo hali ya mambo itasalia kuwa tete kwenye eneo hilo.

Inakadiriwa mkwamo huo uhuenda ukazalisha wakimbizi wengi zaidi hadi kufikia milioni moja hadi ifikapo majira ya kiangazi mwakani.

Akizungumza na waandishi habari, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili katika mataifa ya Lebanon na Jordan, Kamishna wa Guterres alisema kuanzishwa kwa kituo hicho itasaidia kupunguza mkwamo unawaandama wakimbizi hao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter