Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Guinea-Bissau yasikitisha Baraza la Usalama

Hali ya Guinea-Bissau yasikitisha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kusikitishwa kwake na kutokuwepo kwa maendeleo ya dhahiri ya kurejesha utawala wa kikatiba nchini Guinea-Bissau.

Katika taarifa yake, Baraza hilo imesema wajumbe wake 15 wanaamini kuwa utuliv unaweza kurejea kupitia mchakato utakaokubaliwa na pande zote kwa kuzingatia mashauriano ya dhati.

Wajumbe hao wamerejelea azimio namba 2048 la mwaka huu la kutaka kurejeshwa utulivu na kuanza kwa mchakato wa kidemokrasia wa uchaguzi ambapo wametaka litekelezwe.

Halikadhalika wamelaani mashambulio ya kijeshi ya mwezi Oktoba, mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo baada ya mashambulio hayo wananchi wanazuiwa kukusanyika na hata kutoa maoni.

Wameeleza pia wasiwasi wao juu ya ripoti za vitisho dhidi ya watumishi wa Umoja wa Mataiaf na kutaka Guinea-Bissau kuhakikisha usalama wa wafanyakazi hao.