Mkataba mpya wa mawasiliano ya simu wapigia chepuo nchi maskini: IT

14 Disemba 2012

Baada ya wiki mbili za majadiliano, huko Dubai, wajumbe wa mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU wamekubaliana kuhusu mkataba mpya wa mawasiliano ya simu.

Taarifa ya ITU inasema madhumuni ya mkataba huo mpya ni kuwezesha muunganiko wa kirahisi zaidi wa dunia kwa kutumia teknolojia ya kisasa habari na mawasiliano, ICT.

ITU inasema hilo litawezekana kwa kuwa mkataba una vifungu vipya ambavyo vinaweka msisitizo wa masuala kadhaa ikiwemo kuongeza jitihada za kusaidia nchi zinazoendelea, kuwezesha watu wenye ulemavu kunufaika na teknolojia ya mawasiliano pamoja na msisitizo ya kwamba watu wote wana haki na uhuru wa kujieleza kupitia mitandao ya mawasiliano.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud