Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapokea fedha za kufadhili huduma kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha

IOM yapokea fedha za kufadhili huduma kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea dola 700,000 pesa za Canada kufadhili shughuli za misaada kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha. Kulingana na ripoti IOM kwa ushirikiano na idara ya kijamii na maendeleo DSWD juma hili ilitoa msaada wa makao ya dharura kwa familia 600 au watu 30,000 ambao wamekuwa wakiishi nje tangu tufani hiyo kupiga kisiwa na Mindanao tarehe nne mwezi huu.