Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mdororo wa uchumi duniani wazidi kuathiri nchi za Asia-Pasifiki: ESCAP

Mdororo wa uchumi duniani wazidi kuathiri nchi za Asia-Pasifiki: ESCAP

Mdororo wa kiuchumi duniani unazidi kuendelea kuathiri maendeleo ya nchi za Asia na Pasifiki ambapo taarifa hizo ni kwa mujibu wa makadirio mapya ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia-Pasifiki, ESCAP.

Makadirio hayo yaliyotolewa leo huko Thailand yanaonyesha kuwa ukuaji uchumi katika nchi tajiri umeendelea kudorora kwa mwaka 2012 na hivyo kupunguza mahitaji ya bidhaa zinazotengenezwa kutoka nchi za Asia na Pasifiki.

Dkt. Noeleen Heyzer ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mku wa Umoja wa Mataifa na pia Katibu Mtendaji Mkuu wa ESCPA amesema sambamba na athari zitokanazo na mgogoro wa kiuchumi kwa nchi za Ulaya zitumiazo sarafu ya EURO, nchi za Asia na Pasifiki pia zinaweza kuathiriwa pia na makubaliano yoyote yatakayopitishwa na serikali ya Marekani wa kujikwamua na mgogoro wa kiuchumi.