Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zaongeza mauzo yao ya nje: UNCTAD

Nchi zinazoendelea zaongeza mauzo yao ya nje: UNCTAD

Takwimu za mwaka 2012 zilizochapishwa hii leo za shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuongezeka kwa mchango kutoka kwa nchi zinazoendelea kwa uchumi wa dunia kutokana hasa na uundaji wa meli na vifaa vya electroniki. Yakiongozwa na mataifa yaliyostawi ya Asia, mataifa yanayoendelea yameongeza mchango wao kwa mauzo ya nje ya dunia kwa miongo kadha iliyopita.

Mwaka 2011 mauzo ya bidhaa kutoka kwa mataifa hayo yalichangia asilimia 40.4 ya mauzo yote ya dunia huku mataifa ya Korea Kaskazini, China na India yakiongoza. Kati ya bidhaa zinazouzwa na mataifa hayo ni pamoja na tarakilishi na bidhaa za vyombo vya mawasiliano kwenye mauzo yaliyochukua asilimia 60 ya mauzo yote duniani mwaka 2010-2011.