Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la Sudan Kusini lijizuie linapokabiliana na raia: UM

Jeshi la Sudan Kusini lijizuie linapokabiliana na raia: UM

Umoja wa Mataifa umelitaka jeshi la Sudan Kusini kujizuia pindi linapokabiliana na raia.

Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kimetoa taarifa hiyo kufuatia matukio ya hivi karibuni ya mapambano kati ya waandamanaji na polisi yaliyosababisha vifo vya raia Tisa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Taarifa hiyo imesema kwa sasa UNMISS inachunguza chanzo cha matumizi ya nguvu katika matukio hayo kwenye mji mkuu wa jimbo la Bahr El Ghazal wakati huu ambapo tayari bunge la Sudan Kusini limeunda kamati kuchunguza tukio hilo na kutoa mapendekezo yatakayorahisha uchunguzi wa kimahakama.

Halikadhalika, UNMISS imetaka mamlaka nchini Sudan kuchukua hatua za haraka kuzuia mwendelezo wa ghasia na kuwawajibisha wahusika iwapo itabainika nguvu ya kupita kiasi ilitumika dhidi ya waandamanaji.