Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yatupilia mbali rufani ya rais wa zamani wa Ivory Coast

ICC yatupilia mbali rufani ya rais wa zamani wa Ivory Coast

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC, wametupilia mbali madai yaliyotolewa na upande wa utetezi wa aliyekuwa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo waliodai kuwa majaji hao hawakustahili kuendesha kesi hiyo.

Mawakili wanaomtetea Gbagbo waliwalisiha rufani kwenye mahakama hiyo wakidai kuwa majaji wanaoendesha kesi hiyo wanakosa nguvu za kisheria kuendesha kesi hiyo kwa vile Ivory Coast siyo mwanachama wa mahakama hiyo.

Bwana Gbagbo anakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu, matukio ambayo yalijiri baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita.

Katika maamuzi yao, jopo la majaji lililosikiliza furani hiyo ilitupilia mbali madai hayo na kusisitiza kuwa Bwana Gbagbo ataendelea kuwa mikononi mwa mahakama hiyo.