Licha ya mafanikio safari bado ni ndefu kufikia usawa wa kijinsia: WU

13 Disemba 2012

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya uchumi na kijamii, Wu Hongbo amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kufikia usawa wa kijinsia licha ya hatua zilizofikiwa kutokana na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia.

Akizungumza katika mahojiano mjini Geneva, Uswisi, kabla ya mjadala kuhusu mbinu za kuimarisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, Wu amesema kazi bado inahitajika kufanyika.

(SAUTI YA WU)

Washiriki wa mjadala huo wa siku mbili wanajadili pamoja na mambo mengine jinsi usawa wa kijinsia na ajenda ya kuendeleza wanawake inaweza kujumuishwa katika ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo na pia katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter