Ushirikiano njia pekee ya kulinda raia: UNAMID

13 Disemba 2012

Kaimu Mkuu wa kikundi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kinacholinda amani huko Darfur, UNAMID, Aïchatou Mindaoudou amesema ushirikiano miongoni mwa pande zote husika kwenye eneo hilo ndio njia pekee ya kuwezesha ulinzi wa raia.

Bi. Mindaoudou amesema hayo baada ya ziara yake ya siku mbili katika maeneo ya Kusini na Mashariki mwa Darfur ambapo alipata fursa ya kuzungumza na viongozi wa kijamii, serikali na kuchunguza njia mpya za kuendeleza amani na kuimarisha ushirikiano kati ya UNAMID na washika dau uwote.

Amesema ushirikiano mathalani kati ya mamlaka za serikali na viongozi wa kijamii ni muhimu katika kufanikisha mkakati wa UNAMID wa kulinda raia hususan kwa kuepusha matatizo na kuchukua hatua haraka pindi mgogoro unapojitokeza.

Ziara kama hiyo aliifanya mwezi uliopita huko Darfur ya Kati, Magharibi na Kaskazini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud