Wanawake wanaoishi na virusi vya HIV wana nafasi kubwa ya kusaidia juhudi za dunia kukabiliana na kasi ya maambukizi mapya

12 Disemba 2012

Ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI UNAIDS imesema kuwa dunia inaweza kupiga hatua kubwa kukabiliana na tatizo la kuenea kwa virusi vya ugon jwa huo iwapo wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi wakapewa nafasi ya kusikika.

Ripoti hiiyo yenye kichwa cha habari kisemacho, sauti ya wanawake, imeorodhesha mafanukio yaliyojitokeza ambako makundi ya wanaharakati wanawake wamekuwa mstaari wa mbele kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake ndiyo waathirika wakubwa wa UKIMWI na mara nyingi vifo vingi vinavyoripotiwa asilimia kubwa ni ya wanawake.

Ripoti hiyo imesema kuwa, kuwepo kwa ushiriki mkubwa wa wanawake, kuondosha vitendo vya unyanyasaji ni baadhi ya mambo yanaweza kusaidia pakubwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Viwango vya maambukizi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 15 hadi 24 inaelezwa kuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na ile ya vijana wa kiume, hatua ambayo inaonyesha changamoto kubwa inayowakabili wanawake kwa ujumla.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter