Kamati ya UM juu ya haki za watoto yaalani kuendelea matukio ya kunyongwa watoto Yemen

12 Disemba 2012

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto Jean Zermatten, amelaani na vikali tukio la kunyongwa kwa mtoto mmoja wa kike Hind Al-Barti akisema kuwa kitendo hicho kilichotekelezwa mwezi huu mjini Sana’a nchini Yemen ni ukiukwaji mkubwa wa mikataba ya Umoja wa Mataifa.

Duru zinasema kuwa mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka 15 hivyo kupitishwa kwa adhabu ya kunyongwa ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa ikiwemo mkataba wa kimataifa juu ya watoto. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter