Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yatoa nyongeza ya dola Milioni 23 kutokomeza Kipindupindu Haiti

UM yatoa nyongeza ya dola Milioni 23 kutokomeza Kipindupindu Haiti

Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa tishio nchini Haiti hali iliyolazimu Umoja wa Mataifa kutoa nyongeza ya dola Milioni 23 zaidi kusaidia vita dhidi ya ugonjwa huo.

Nyongeza hiyo inajazia kiasi cha dola Milioni 118 ambazo Umoja wa Mataifa umeshatumia hadi sasa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo nchini Haiti.

Nigel Fisher ni Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti.

(SAUTI YA NIGEL FISHER)

Haiti inahitaji karibu dola Milioni 500 kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kusaidia mpango wake wa kitaifa wa kujikwamua kutoka katika majanga yaliyoikumba ikiwemo ukame na vimbunga.