Katibu Mkuu alaani kitendo cha DPRK kukiuka azimio la UM

12 Disemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani kitendo cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK cha kurusha roketi hapo jana kinyume na azimio la Umoja huo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amemkariri Bwana Ban akisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa kitendo hicho kimekiuka wito wa jumuiya ya kimataifa na azimio namba 1874 ambalo linazuia DPRK kutumia teknolojia ya masafa marefu katika urushaji wa chomb chochote angani.

Bwana Ban amesema ana wasiwasi kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa na madhara ambayo yanaweza kuchochea vitendo vya kutishia amani na usalama huo Asia na kwamba yeye amejizatiti kuona kuna amani na utulivu kwenye rasi ya Korea. Hivyo ameitaka serikali ya DPRK kutorudia kitendo hicho na badala yake kujiaminisha kwa majirani zake huku ikiimarisha maisha ya wananchi wake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter