Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya usalama, mila na desturi zakwamisha matumizi ya vyoo

Hofu ya usalama, mila na desturi zakwamisha matumizi ya vyoo

Umaskini pamoja na mila na desturi ni baadhi ya mambo yanayosababisha usafi duni miongoni mwa nchi maskini. Usafi huu duni unamulika zaidi matumizi ya vyoo salama ambapo inaelezwa kuwa kutokana na baadhi ya mila baadhi ya watu wanalazimika kujisaidia haja kubwa vichakani na hivyo kuhatarisha kuenea kwa magojwa kama vile kipindupindu.

Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa mwanamke mmoja kati ya watatu duniani kote yuko hatarini kukabiliwa na aibu, magonjwa, manyanyaso na hata shambulio kutokana na ukosefu wa mahali salama pa kujisaidia iwe haja kubwa au ndogo. Je hali halisi ya matumizi ya vyoo ikoje? Tumejikita Burundi ambako mwandishi wetu wa Maziwa Makuu, Ramadhani Kibuga ametembelea mtaa wa Buterere kaskazini mwa mji mkuu Bujumbura.

(PKG YA KIBUGA)