Tumejizatiti kuridhia jeshi kwenda Mali: Baraza Kuu la UM

11 Disemba 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani kitendo cha jeshi nchini Mali kumkamata Waziri Mkuu wa nchi hiyo Cheik Modibo Diarra na kusababisha kujiuzulu kwa serikali.

Taarifa hiyo imesema kitendo hicho ni kinyume na maazimio ya Baraza hilo yanayolitaka jeshi hilo lisiingilie kazi ya mamlaka za mpito nchini Mali.

Kwa kauli moja wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza azma yao ya kuwa tayari kuidhinisha kupelekwa nchini humo kwa jeshi la kulinda la nchi za Afrika kwa usaidizi wa jumuiya ya kimataifa.

Halikadhalika wameelezea utayari wao wa kufikia hatua stahili ikiwemo vikwazo dhidi ya wale wote wanaokwamisha mipango ya kurejesha utawala wa kikatiba nchini Mali.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter