Milima yazidi kuporwa, maisha ya wakazi wake yazidi kuwa duni

11 Disemba 2012

Milima ni tegemeo la wakazi wa dunia kwa shughuli na huduma mbali mbali ikiwemo maji ya kunywa, umwagiliaji, shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii na kadhalika. Hata hivyo maendeleo ya binadamu yamekuwa kikwazo kwa milima kuweza kutoa huduma hizo na hata kuhatarisha maisha ya wakazi au jamii za milimani. Katika siku ya kimataifa ya milima duniani hii leo tarehe 11 Disemba 2012 inaelezwa kuwa milima iko hatarini zaidi hivi sasa na hata maisha ya wakazi wa milimani nayo yanazidi kuwa duni. Je ni kwa nini? Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Richard Muyungi Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter