Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya shule 600 ziliibiwa vifaa au kuharibiwa huko DRC: UNICEF

Zaidi ya shule 600 ziliibiwa vifaa au kuharibiwa huko DRC: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema shule 250 zilizokuwa zinatumika kuhifadhi wakimbizi wakati wa mzozo huko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC zimepora vifaa au zimeharibiwa na hivyo kufanya idadi ya shule zilizoathirika na mzozo huo kufikia 600.

Ripoti ya UNICEF inasema kuwa takribani wanafunzi 240,000 wameshindwa kwenda shule kwa wiki kadhaa sasa kutokana na mzozo huo mashariki mwa DRC ulioanza mwezi Aprili. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)