Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa yazungumzia kuuawa kwa wanafunzi kwenye chuo kimoja mjini Khartoum

11 Disemba 2012

Ofiki ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa hivi majuzi kati ya wanafuzni na polisi mjini Khartoum nchini Sudan. Habari zinasema wanafunzi waliandamana kwa siku tatu mfululizo wakilalamikia vifo vya wanafunzi wannne wa chuo cha El- Gezira kilicho kati kati mwa Sudan.

Hii ni baada ya miili ya wanafunzi hao kupatikana kwenye mtaro mnamo tarehe 7 mwezi huu tangu walipotoweka juma lililopta baada ya kushiriki kwenye maandamano. Wakati huo huo ofisi hiyo ya haki za binadamu imeelezea wasi wasi kutokana na dhuluma zinazoendeshwa dhidi ya watetesi wa haki za binadamu na kuuawa kwa mwandishi wa habari nchini Sudan Kusini siku za hivi majuzi. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud