Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha duni ya wakazi wa milimani, hatua kuchukuliwa kuboresha maisha yao

Maisha duni ya wakazi wa milimani, hatua kuchukuliwa kuboresha maisha yao

Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Richard Muyungi amesema hali ya milima na maisha ya wakazi wake iko hatarini zaidi hivi sasa kutokana na shughuli za binadamu zinazosababisha mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya Milima hii leo, Bwana Muyungi ametaja shughuli hizo kuwa ni ukataji holela wa magogo, matumizi ya kuni kwa ajili ya nishati na shughuli za kilimo kwenye milima.

Amesema mazingira haribifu yanafanya jamii za maeneo hayo kuishi maisha duni na hivyo mkutano wa Doha uliomalizika hivi karibuni umeazimia hatua za kulinda milima.

(SAUTI YA MUYUNGI)

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wote duniani wanategemea maji yatokayo milimani kwa ajili ya matumizi ya kunywa, kupika, uzalishaji na hata umwagiliaji.