Wakiukaji wa haki wawajibishwe: Maafisa UM

10 Disemba 2012

Katika kilele cha kampeni ya siku 16 ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia inayoenda sambamba na siku ya haki za binadamu hii leo, maafisa wa Umoja wa Mataifa wametaja ujumbe unaozingatiwa wakati huu ambao ni pamoja ukweli, haki na uwajibishwaji wa wale wanaokiuka haki hizo.

Maeneo yaliyokumbwa na machafuko ya vita ndiyo yanayolengwa zaidi na kampeni hiyo ambayo imelenga kuwakwamua wanawake wanaoteseka na matukio ya unyanyasaji na kuwapa uhuru na haki.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaozingatia haki za wanawake na uhuru wao Bi Zainab Hawa Bangura na Bi. Rashida Manjoo wamesema kuwa kuanzishwa kampeni hiyo iliyopewa jina la siku 16 za kiharakati kuwatetea wanawake ni mwanga unaotumwa kwa mataifa yote duniani ambayo yanapaswa kukomeshwa vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake. Taarifa Kamili Na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter