Umiliki wa simu za mkononi umepanda katika nchi nyingi zaidi: ITU

10 Disemba 2012

Takwimu za hivi karibuni za shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU, kuhusu hali ya teknolojia duniani zinaonyesha kuwa mwanzoni mwa mwaka 2012, kulikuwa na nchi saba ambako umiliki wa simu za mkononi ulizidi asilimia 200, ikimaanisha kuwa kila mtu alikuwa na zaidi ya simu mbili.

Uchina ndiyo nchi ya kwanza duniani kuwa na watu zaidi ya bilioni moja walio na simu za mkononi, ikifuatiwa kwa karibu na India. Kwa mujibu wa takwimu hizo pia, mapato ya kila mwaka yatokanayao na teknolojia ya mawasiliano yamefika dola trilioni 1.5, au asilimia 2.4 ya mapato ya nchi zote duniani kwa jumla.

Kati ya mwaka 2008 na 2011, gharama ya huduma za teknolojia ya mawasiliano ilishuka kwa asilimia 30. Hata hivyo, thuluthi tatu za vijana chini ya miaka 25, ambayo ni idadi ya watu takriban bilioni mbili, bado hawana uwezo wa kuwa kwenye mitandao ya mawasiliano.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter