Mkurugenzi mkuu wa ILO aelezea wasi wasi wake kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Tunisia

10 Disemba 2012

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder ameelezea wasi wasi wake kutokana na matukio ya hivi majuzi ambayo yameshuhudiwa nchini Tunisia hasa ghasia zinazoendeshwa dhidi ya viongozi wa vyama vya wafanyikazi na ofisi za chama cha wafanyikazi nchini Tunisia (UGTT).

Bwana Ryder amesisitiza kuwa mashirika ya wafanyikazi na yale ya waajiri hayawezi kutekeleza haki zao kwenye mazingira yenye ghasia na vitisho dhidi ya viongozi au wanachama wao. Amesema kuwa ni lazima serikali ilitilie maanani suala hili na ihakikishe kuwa chochote kinapotokea ni lazima ifanye uchunguzi na kuwachukulia hatua wanahusika na kuzuia kurudiwa kwa vitendo kama hivyo. Ryder pia ametoa wito kwa utawala nchini Tunisia kufanya jitihada ili kuvihakikishia haki vyama vya wafanyikazi kwa kuwa ndio msingi wa mazungumzo ya kutafuta suluhu wakati wa mizozo.

.