Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapatiwa mapendekezo ya kuimarisha uwezo wa MONUSCO

Baraza la Usalama lapatiwa mapendekezo ya kuimarisha uwezo wa MONUSCO

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limepatiwa mapendekezo ya awali ya kile ambacho kinapaswa kufanywa ili kuimarisha uwezo wa kikosi cha umoja huo kinacholinda amani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, MONUSCO, suala ambalo linatokana na azimio 2076 lililopitishwa mwezi uliopita na baraza hilo. Azimio hilo lilipitishwa baada ya waasi wa M23 kuingia na kuchukua mji wa Goma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mpango huo, Msimamizi mkuu wa shughuli za ulinzi wa amani kwenye umoja huo Herve Ladsous amesema wameandaa mapendekezo hayo baada ya ziara ya mshauri mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu masuala ya kijeshi Jenerali Babacar Gaye kutembelea mashariki mwa DRC.

Amesema hali ni shwari kwa sasa licha kuwepo kwa baadhi ya wafuasi wachache wa waasi wa M23 huko Kivu Kaskazini lakini askari wa MONUSCO na polisi wa serikali wanaendelea kufanya doria.

Kwa mujibu wa Ladsous, wametoa mapendekezo matatu juu ya kuimarisha uwezo wa MONUSCO kwa ajili ya kuzingatiwa na baraza la usalama.

(SAUTI YA LADSOUS)