Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa mishahara wapungua duniani licha ya kuongezeka katika nchi zinazoendelea: ILO

Ukuaji wa mishahara wapungua duniani licha ya kuongezeka katika nchi zinazoendelea: ILO

Ripoti ya shirika la kazi Ulimwenguni ILO imeonyesha kuwepo kwa ongezeko ndogo la ukuaji wa ujira na wakati huo hali katika nchi zilizoendelea siyo ya kuridhisha licha maeneo hayo kushuhudia kuanza kuimarika kwa hali ya uchumi baada ya kukubwa na misuko suko ya kuanguka kwa uchumi.

Ripoti hiyo ya mwaka 2012-2013 iliyotolewa leo inaonyesha kuwa hali ya ujira kwa mwezi iliongezeka kwa asilimia 1.2 mwaka 2011, ikiwa ni anguko la asilimia 3 ikilinganishwa na kiwango kilichorekodiwa mwaka 2007. Pia inaelezwa kuwa kiwango hicho cha ukuaji kinaweza kushuka zaidi kama takwimu hizo hazitahusisha China. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)