Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awasili Uturuki, atarajiwa kuzuru kambi ya wakimbizi wa Syria

Ban awasili Uturuki, atarajiwa kuzuru kambi ya wakimbizi wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili nchini Uturuki ambako anatarajiwa kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Tayyip Erdogan na Waziri wa Mambo ya Nje, Ahmet Davutoglu.

Katika ziara hiyo, Bwana Ban anatarajiwa kuzuru baadhi ya kambi za wakimbizi wa Syria ambao wamekimbilia usalama wao nchini Uturuki, kufuatia machafuko yalodumu miezi ishirini nchini mwao.

Takriban wakimbizi 465,000 wa Syria wamekimbilia nchi jirani katika Mashariki ya Kati, zikiwemo Uturuki, Iraq, Jordan na Lebanon.