UM na WEF wazindua mpango wa kuwepo kwa mbinu za uwekezaji ambazo ni rafiki kwa mazingira

7 Disemba 2012

Umoja wa Mataifa kupitia sekretarieti yake ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na Kongamano la kidunia la uchumi, WEF wamezindua mpango mpya ujulikanao kama Msukumo wa mabadiliko,uwekezaji fedha katika vitegauchumi rafiki kwa mazingira.

Ushirikiano huo umetangazwa huko Doha, Qatar ambako mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi umemalizika leo na lengo la mpango huo ni kutamba miundo ya uchangishaji fedha za uwekezaji unaopunguza athari za mazingira kwenye nchi zinazoendelea.

Katibu Mtendaji wa UNFCCC Christiana Figerese amesema watamulika mbinu za ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwenye nchi zinazoendelea ambazo zinapatia majibu matatizo ya mabadiilko ya tabia nchi.

Amesema mbinu hizo zitaweza kuwa mfano kwa serikali, sekta ya biashara na viwanda kama vichocheo vya kuwa na vitegauchumi rafiki kwa mazingira.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter