Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo dhidi ya magonjwa ya Surua na polio yanendelea nchini Syria

Chanjo dhidi ya magonjwa ya Surua na polio yanendelea nchini Syria

Kampeni ya dharura ya kutoa chanjo kwa sasa inaendelea nchini Syria kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa surua na polio ikiwa inawalenga watoto milioni 1.4. Kampeni hiyo inaongozwa na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na jumla ya chanjo milioni 1.5.

UNICEF inasema kuwa hakujakuwa na hakikisho kutoka kwa pande zinazozozana iwapo kampeni hiyo itaendelea bila kutatizwa na mapigano lakini hata hivyo kuna dalili za kuvurugwa kwa kampeni hiyo. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MARECADO)