Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea mshangao wake na ghasia zinazoendelea nchini Misri

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea mshangao wake na ghasia zinazoendelea nchini Misri

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasi wasi wake kutoakana na kunelea kwa kizozo na mauaji kwenye maanbamano ya kupinga katiba nchini Misri ambayo inatarajiwa kuadhinishwa tarehe 15 mwezi huu.

Bi Pillay amekaribisha wito wa rais Muhammed Morsi wa kutaka kufanyika kwa mazungumzo lakini akajutia kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuhusiana na utata unaoikumba katiba. Msemaji kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Rupert Colville amesema kuwa ofisi ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiyachambua yaliyo kwenye katiba hiyo na kufutia kwa karibu kuandikwa kwake.