Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahitaji dola Milioni Saba kwa ajili ya usaidizi Ufilipino

IOM yahitaji dola Milioni Saba kwa ajili ya usaidizi Ufilipino

Takribani watu Laki Tatu na Nusu wanaishi katika vituo vya hifadhi huko Mashariki mwa kisiwa cha Mindanao nchini Ufilipino baada ya kimbunga Bopha kuharibu makazi, mali na miundombinu pamoja na kusababisha majeruhi na vifo vya watu takribani 500.

Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM linasema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka na kiwango cha uharibifu sasa kiko dhahiri ambapo maelfu ya watu hawana makazi na wengine hawajulikani waliko.

IOM imesema kufuatia ombi la serikali tayari imepeleka watendaji wake Mindanao kusaidia kusambaza misaada ya vifaa na ukarabati wa makazi na sasa inaomba dola Milioni Saba kusaidia kukidhi mahitaji ya kibinadamu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE )