Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Assad wa Syria akabiliwe na sheria iwapo atatumia silaha za kemikali: Ban

Rais Assad wa Syria akabiliwe na sheria iwapo atatumia silaha za kemikali: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kwamba rais wa Syria Bashar al-Assad atawajibika kisheria iwapo serikali yake itatumia silaha za kemikali kukabiliana na upinzani nchini Syria.

Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad, Iraq, ambako amekutana pia na Waziri Mkuu, Nuri al-Maliki. Bwana Ban amesema ameelezea hofu yake kwa serikali ya Syria, na pia katika waraka alomtumia rais Assad.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Bwana Ban pia amezungumzia uhusiano uliopo kati ya Iraq na Kuwait, akisema sasa uhusiano huo umeimarika, na kwamba wakati umewadia wa nchi hizo mbili kusahau yalopita na kukaribisha enzi mpya ya ushirikiano.