Makubaliano ya kulinda na kusaidia wanaohama yaanza kutekelezwa

6 Disemba 2012

Makubalano ya Muungano wa Afrika kuhusu usalama na misaada kwa wakimbizi wa ndani yanayojulikana pia kama makubaliano ya Kampala yameanza kutekelezwa hii leo baada ya jumla ya mataifa 15 kuyaunga mkono. Makubaliano hayo yanatoa mpangilio wa kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi wa ndani na kuyataka mataifa ya Afrika kuzuia uhamiaji .

Kamishna mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres amesema kuwa kutekelezwa kwa makubaliano hayo ni hatua ya kihistoria ya kuwalinda karibu wakimbizi milioni moja walio barani Afrika. Msemaji wa UNHCR Fatoumata Lejeune-Kaba anasema kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na mafuriko ndiyo chanzo cha uhamiaji barani Afrika.

Kwetu sisi itasaidia kuboresha njia za kuwafikia wakimbizi kwa njia iliyo nzuri na hii inategemea na kujitolea kwa serikali. Tuna matumaini kuwa hii inamaanisha kuwa wakati kuna uhamiaji tutaruhusiwa kuenda kufanya tathmini na kutoa huduma zinazohitaji. Hii inaweza kusaidia kuzuiai hali ngumu ya kibinadamu na pia inamaanisha kuwa itazuia kuhama kwa watu. Kwa sababu wakati tuna uwezo wa kufikia sehemu ambazo watu wameanza kuhama tusaidie, watu wanaweza kukaa na wako karibu na nyumbani. Wakati hamna msaada wa kibinadamu kwa muda watu uhamia maeno mengine na hali ya kibinadamu hudorora.