Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yataka mataifa kuelekeza asilimia kubwa ya uwekezaji kwenye kilimo

FAO yataka mataifa kuelekeza asilimia kubwa ya uwekezaji kwenye kilimo

Uwekezaji ulio bora kwenye kilimo ni moja ya njia madhubuti za kuangamiza njaa na na umaskini na pia kulinda mazingira. Hii ni kwa mujibu wa ripoti yenye kichwa “Hali ya chakula na kilimo mwaka 2012” iliyotolewa hii leo mjini Rome.

Ripoti hiyo inasema kuwa wakulima zaidi ya bilioni moja duniani wanastahili kupewa kipaumbele katika uwekezaji wowote wa kilimo kwa kuwa ndio wawekezaji wakubwa kwenye sekta hii. Kulingana na Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva ni kwamba mikakati mipya inahitajika ya kuwapa kipaumbele wakulima.