Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yatakiwa kuheshimu makubaliano yaliyomaliza mapigano Gaza

Israel yatakiwa kuheshimu makubaliano yaliyomaliza mapigano Gaza

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kwenye maene ya kipalestina yanayokaliwa na Israel tangu mwaka 1967 Richard Falk ametoa wito kwa Israel akiitaka itekeleze makubaliano yaliyositisha mzozo kwenye ukanda wa Gaza. Falk aliyasema hayo alipofanya ziara kwenye ukanda wa Gaza na Misri ambapo alikutana na waakilishi wa mashirika ya umma na serikali pamoja na waathiriwa wa ghasia zilizoshuhudiwa. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)